Serikali
ya Jamhuri ya Burundi imesema ipo tayari kutoa ushirikiano wa hali na
mali katika kuhakikisha zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi waliopo nchini
Tanzania wanarejea nchini Burundi kwa haraka ili wakaijenge nchi yao.
Haya
yamezungumza na Waziri wa mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka
Jamhuri ya Burundi Mhe. Pascal Barandagiye, alipozuru katika kambi za
Nyarugusu, Nduta na Mtendeli kutoa ujumbe wa kuwaasa kurejea wakimbizi
nchini kwao Burundi.
Tangu
zoezi la urejeaji wa wakimbizi lilipoanza mwezi septemba 2017 kwa awamu
ya kwanza jumla ya wakimbizi 8347 wameshasaidiwa kurejea nchini kwao
Burundi sawa na asilimia 100.3 ya lengo ya urejeshwaji kwa awamu ya
kwanza.
Aidha,
mwanzoni mwa mwezi Novemba wakimbizi wapatao 33,948 walijiandikisha
kurejea nchini kwao Burundi lakini kutokana na kasi ndogo na taratibu
ndefu zinazofanywa na Shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani UNHCR
wakimbizi waliojiandikisha wameanza kusitisha nia yao ya kurejea kwani
hawaoni jitihada zinazofanywa kuwarudisha, ambapo jumla ya wakimbizi 735
kati ya 33948 wamesitisha nia yao ya kureja kwa hiari.
Hali
hii inatajwa na viongozi wa Burundi kuwa inachelewesha zoezi kwani
wakimbizi wanaorejeshwa kwa mujibu wa mpango wa urejeaji ni ndogo. Mhe.
Pascal Barandagiye amesema serikali ya yake ipo tayari kutoa magari
kwaajili ya kuwasafirishwa wakimbizi kurudi nchi mwao, pamoja na kuwapa
huduma muhimu za kibinadamu.
“zoezi
la urejeshaji wa Wakimbizi kwa hiari linaenda polepole mno tofauti na
matarajio, shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR linaenda kwa
kasi ndogo tofauti na ilivyotarajiwa, hivyo kutokana na zoezi
hilonkuenda taratibu Serikali ya Burundi ipo tayari kutoa magari, fedha
na huduma nyingine za kibinadamu ili kusaidia kuweza kuharakisha zoezi
la kurejesha wakimbizi waliojiandikisha kurejea kwa hiari nchini
Burundi” alisisitiza Barandagiye.
Akiongea
katika nyakati tofauti tofuti katika kambi za nyarugusu, nduta na
mtendeli, amewahakikishia wananchi wa kuwa Amani nchini mwao ipo ya
kutosha hakuna vurugu na serikali ya Burundi inawahitaji ili warejee
kuenga taifa lao hakuna haja ya kuendelea kubaki makambini.
Wakimbizi
wakiongea kwa nyakati tofauti wamemhakikishia kuwa bado wanapenda nchi
yao Burundi, na wanatamani kurejea Burundi, lakini changamoto
inayowakabili hadi kukata tamaa ya kurudi ni taratibu ndefu
zinazowachelewesha kurejeshwa mara tu baada ya kujiandikisha
Akiongea
kwa niaba ya Wakimbizi walioko kambi ya Nduta Bw. Suleima Hamisi (65)
ambaye amekuwa Mkimbizi mara Sita kwa nyakati tofauti tangu mwaka 1972
alisema “ Sisi tulishajiandikisha Zaidi ya miezi mine sasa ili tuweze
kurejeshwa cha kushangaza hadi sasa badotupo makambi” ameiomba serikali
ya Burundi na Tanzania na Shirika la kuhudumia wakimbizi wakae na
kuzungumza kwa pamoja juu ya mustakabali wa kuwarejesha haraka wenye nia
ya kurudi Burundi.
Akitoa
taarifa kwa Waziri wa mambo ya ndani na mafunzo ya uzalendo wa Burundi
na Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania,
Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu ikiyopo Wilayani Kasulu alisema kumekuwa na
mwitikio Mkubwa wa wakimbizi wanao jiandikisha kurejea kwa hiari nchini
Burundi lakini changamoto imekuwa taratibu ndefu zinazochelewesha
kurejea kwao zinawafanya baadhi yao kuahirisha kurejea kutokana na
kusubiri kwa muda murefu.
Serikali
ya Burundi pia imedai Shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR
linatakiwa kubadilisha utaratibu wa kuwapatia au kuwagawia vyakula na
pesa wakimbizi wanapokuwa wanarejea wameomba zoezi hilo lifanyike wakati
tayari wakimbizi wakishapatiwa nyumba na maeneo yao ya makazi kuepusha
kukaa kwa muda mrefu kwenye vituo vya kuwapokelea.
Naye
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema
serikali ya Tanzania itahakikisha wakimbizi waliopo nchi wanahifadhiwa
kwa mujibu wa makubaliano ya taratibu za kimataifa na wale wanaopenda
kurejea kwa hiari itashirikiana na UNHCR, nchi ya Burundi ili
kufanikisha zoezi hilo. Hatua ya kuwarejesha wakimbizi katika nchi yao
ya asili ni moja kati ya suluhisho la kudumu la ukimbizi kwa mujibu wa
sharia ya kimataifa ya wakimbizi ya mwaka 1951 na Sheria ya Wakimbizi ya
Tanzania yam waka 1998 kifungu Na. 3
Zoezi
la kurejea kwa wakimbizi nchini mwao waliopo Tanzania lilianza
kuratibiwa mara tu baada ya tamko la viongozi rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya
Burundi Pierre Nkurunzinza walipo kutana Mwezi Julai 20, 2017 na kutamka
kuwa wakimbizi waliopo Katika Makambi nchi Tanzania warejee nchini kwao
kwani Burundi kuna amani ya kutosha.
Hadi
sasa idadi ya wakimbizi walioko katika Mkoa wa Kigoma ni 210,005 na
waomba hifadhi 26,410, kati ya hao 95,243 wapo kambi ya Nduta, 48147
kambi ya Mtendeli na 66615 Nyarugusu, aidha waombahifadhi wote wapo
katika kambi ya nduta.







No comments:
Post a Comment