Waziri Mkuu Abaini Semi Trela 44 Zikitaka Kutolewa Bandarini Bila Yakufuata Utaratibu....Amtaka IGP Sirro Awakamate Wahusika

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro kuwakamata, Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw. Samwel kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya semi tela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Pia Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu Serikalini.

“Mtu asije hapa aseme amepewa kibali na Rais Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu cha kutaka kutoa mzigo wake bila ya kufuata taratibu. Akija mtu na taarifa hizo akamatwe mara moja na achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.”

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Novemba 29, 2017) alipofanya ziara ya ghafla bandarini baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuutapeli uongozi wa TPA kutaka kutoa magari hayo yaliyoingizwa nchini mwaka 2015 kutoka nchini Uturuki.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bw. Bahman wa kampuni ya NAS kutaka kupata msamaha wa  kodi kwa kuidanganya TPA kwa madai kwamba wamewasiliana na Waziri Mkuu na wasipotekeleza jambo hilo watapata matatizo.

Amesema Serikali inasisitiza watu kufuata sheria na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kulipakodi  ipasavyo na inataka watendaji wake wafanye kazi bila ya kubugudhiwa, hivyo amewataka wafanyabiashara kufuata sharia za nchi na kwamba Serikali haina ugomvi nao.

Waziri Mkuu amefafanua kuwa mfanyabiashara huyo alitaka kuyatoa magari hayo bila ya kukamilisha malipo ya ununuzi kutoka kwenye kampuni Serin ya nchini Uturuki.

“Magari haya aliyalipia asilimia 30 tu kwa makubaliano ya kumaliza asilimia 70 iliyobaki baada ya kufika Tanzania na atakapokamilisha ndipo angepewa nyaraka ambayo inaonyesha jina la mwenye mzigo, aina ya mzigo na thamani  (bill of lading) inasaidia mteja kufanyiwa tathmini ya gharama za kulipia ushuru, lakin huyu bwana hajafanya hivyo”

Waziri Mkuu amesema kitendo cha kuyasajili magari hayo bila ya kuwa na nyaraka hizo ni kinyume cha sheria na pia kinaweza kusababisha kampuni iliyouza magari hayo ya Serin kutolipwa malipo yaliyobaki. 

Amesema jambo hilo halikubaliki kwa sababu linaweza kudhohofisha mahusiano mazuri iliyopo kati ya Tanzania na Uturuki kwani tayari kampuni hiyo imeshawasilisha malalamiko hayo katika ofisi za Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania.

“Uturuki wanawaamini sana wafanyabiashara wa Tanzania sasa huu ujanjaunja uliotumika katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuyasajili magari haya bila ya kuwa na bill of lading halisi unajenga sura mbaya kwa wafanyabiashara wengine waaminifu na watiifu wa sheria nawaagiza TRA kuchukua hatua kwa wahusika, hatuwezi kupoteza mahusiano na nchi kwa sababu ya utapeli wa mfanyabiashara mmoja.”

Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa Mawakala wa Forodha kuhakikisha wanakuwa makini katika kazi zao na Serikali haitawavumilia wababaishaji kwani inasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.

Awali, Mkurugenzi wa Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko alimueleza Waziri Mkuu kuwa pamoja na vitisho vya mfanyabiashara huyo kuwa wasipotekeleza matakwa yake watapata matatizo, lakini waliendelea kusimamia sheria na taratibu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, NOVEMBA 29, 2017
Share:

KAMANDA SIRO AJIGAMBA KUUPUNGUZA MTANDAO WA MAJANGILI WALIOKUWA WAKIUWA KIBITI,

MKUU wa jeshi la polisi nchini (IGP)Simon Sirro amewahakikishia wananchi mkoani Pwani kuwa silaha zote zilizochukuliwa na wahalifu wa ovyo ovyo huko Kibiti na Mkuranga zimerudi zote mkononi mwa dola na kusambaratisha mtandao wa kiuhalifu .
Aidha ametoa rai kwa wazazi na walimu kutoa taarifa kwenye vituo vya polisi mara watakapobaini kuna mwanafunzi mtoro ama hajaripoti shule kwa miezi kadhaa kwani wapo baadhi ya watoto wanaotumika kufundishwa uhalifu hata wakutumia silaha na watu wasiowema.
 
Pamoja na hayo IGP Sirro ,amesema vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinashirikiana na nchi ya Msumbiji kupambana na wahalifu waliobainika kukimbilia nchini  humo wakitokea Tanzania.
 
Aliyasema hayo wilayani Kibaha ,mkoani Pwani ,katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo pia alizungumza na viongozi wa mashirika ya umma,wazee maarufu ,wastaafu mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapo.
 
IGP Sirro alieleza kuwa ,vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kupambana na yeyote atakaekuja kwa moto nae wataenda nae kwa moto na atakaekuja baridi wataenda nae baridi.
 
Alisema serikali imeshinda kwa hilo na hali kwa sasa ni shwari katika wilaya hizo.
 
IGP Sirro alieleza amepatiwa taarifa ya wanafunzi zaidi ya 1,300 mkoani hapo kuwa ni watoro na hawajulikani walipo hivyo wazazi washirikiane kusaidia jeshi la polisi kujua walipo.
 
“Kuna baadhi misikiti,makanisa yanadaiwa yanayotumia watoto hawa katika masuala ya kiuhalifu hivyo kuna kila sababu ya kuingia ndani kutafuta suluhu “
 
“Ni kazi yetu wazazi jamii na walimu kushirikiana ,na hapa ni muhimu wazazi wasaidie kusema watoto wao walipo ili kuwa na usalama” alisema .
 
Katika hatua nyingine IGP Sirro alielezea viongozi wa dini wana nafasi ya kuhakikisha wanatumia eneo lao kuhubiri amani .
 
“Tusidharau taarifa hata kama ni ndogo ,tusibweteke umoja ni nguvu tusaidiane kukomesha vitendo vya uvunjifu wa amani ” alifafanua IGP Sirro.
 
Akizungumzia changamoto ya wahamiaji haramu alisema wanashirikiana na uhamiaji kuusaka mtandao unaohusika kufanya biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu .
 
IGP Sirro alisema hawatamvumilia yeyote anaekumbatia wahamiaji haramu kwani ni chanzo cha kusababisha kuleta magaidi  na kusafirisha bidhaa za haramu .
 
Alisema kwasasa wamejipanga kutaifisha mali za wafanyabiashara hao wa wahamiaji haramu na usafiri utaotumika kuwasafirisha.
 
Nae mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,ameshukuru kuwepo Kwa kanda maalum kwani imeweza kuleta mafanikio makubwa .
 
Alisema kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya sintofahamu ,watu walisitiza shughuli zao za maendeleo ,biashara zilikwama,watu na baadhi ya viongozi walihama nyumba zao na wengine kulala saa 12 jioni kwa kuhofia mauaji.
 
Mhandisi Ndikilo alieleza sasa Kibiti na Rufiji hali ni shwarii kutokana na kuimarishwa ulinzi.
 
Aliwataka pia wawekezaji na wadau mbalimbali mkoani Pwani ,kujitokeza kushirikiana kusaidia kutatua changamoto zinazolikabili jeshi la polisi ikiwemo uhaba wa vitendea kazi ,usafiri na kujenga vituo vya polisi .
 
Mhandisi Ndikilo, alisema kuwa Mkoa huo umesheheni viwanda vya kutosha hivyo ni vyema kusaidia mambo hayo kwa manufaa ya wote wakati kukitokea uhalifu.
 
“Tukikumbwa na uhalifu tunapigia simu polisi, tusiwe Wa kwanza kulaumu wakati wa matatizo ,tukumbuke na kuwasaidia ili kufanikisha kazi zao kifanisi.;:” alisema mkuu huyo wa mkoa .
 
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani Pwani ,(ACP)Jonathan Shanna alisema ziara hiyo ni neema kwao na wamepewa maagizo mbalimbali ambayo watayafanyia kazi.
 
Kamanda Shanna alisema wamemfikishia kero IGP zinazowagusa askari polisi ikiwemo upungufu wa makazi .

Advertisement
Share:

KENYATTA KUAPISHWA RASMI KUWA RAISI MPYA WA NCHI HIYO BAABA YA MVUTANO NA REILA ORDINGA.


Ni siku nyingine ambayo Taifa la Kenya leo linatekeleza shughuli muhimu ya kikatiba ya kumuapisha kiongozi wa taifa hilo kufuatia ushindi wake wa marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 uliosusiwa na upinzani.

Uhuru Kenyatta leo anaapishwa rasmi kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa pili baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu.

Wageni mbalimbali wanatarajiwa kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa kiongozi huyo wa Kenya huku ulinzi ukiimarishwa kila kona

Uchaguzi wa  uliofanyika Agosti ulifutwa  na mahakama kutokana na kile kilichotajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki.

Marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa  na asilimia 39.

==>Tazama tukio hilo hapo chini


 
Share:

Makamu wa Rais Samia Suluhu amuwakilisha Rais Magufuli nchini Kenya Kushuhudia Kuapishwa kwa Rais kenyatta.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana.

Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Nairobi

28 Novemba, 2017
Share:

WAKATI IMEAKIA SIKU MOJA KURUDIA MNADA WA NYUMBA ZA LUGUMI, YONO AUCTION MART WATOA TAMKO,


Kampuni ya Udalali ya Yono imetangaza kuwa kesho, Novemba 24, 2017 itarudia upya mnada wa nyumba mbili za kifahari za mfanyabiashara Said Lugumi zilizoshindikana kuuzwa baada ya Dr. Louis Shika kuzinunua na kushindwa kuzilipia.

Nyumba zilizotajwa kurudiwa kuuzwa katika mnada ni Plot. No 47, iliyopo Mbweni JKT,  na nyingine iliyopo Upanga

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart, Scholastica Kevela ameeeleza kuwa kwa sasa kampuni ya Yono imeweka masharti magumu ili kuhakikisha kwamba hakuna atakayeibuka kuuharibu mnada huo.

“Niwakaribishe wateja ndani na nje ya nchi kuja kujinunulia nyumba zile kwa maana ujenzi ni mgumu..” amesema.

Aidha Bi Scholastica Kevela amewaonya wale wote wenye nia ya kuuharibu mnada huo kutofanya hivyo kwani hawatavumiliwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Niseme kwamba mchezo ule tuliochezewa mara ya mwisho hautarudiwa tena. Kwa sasa hivi tumekuja na masharti magumu kwamba washiriki wote wawe aware na wanielewe,” amesema Bi. Kevela.

Masharti yaliyowekwa katika minada hiyo ni kwamba mshiriki atapaswa kujiandikisha kwenye kitabu maalum cha washiriki wa minada, baada yahapo atajaziwa ‘commitment form’ (fomu maalumu ya kushiriki mnada).

Baada ya hayo, vitambulisho vya mshiriki ikiwemo hati ya kusafiria (passport), leseni ya udereva na kitambulisho cha mpiga kura vitachukuliwa na kampuni.

Kila mshiriki halali atapaswa kulipa kiasi cha shilingi milioni 2 kupitia akaunti ya Yono ili kuthibitisha kuwa ana lengo la kushiriki. Kwa atakayeshinda mnada, fedha hizo (sh. 2 milioni) zitatumika kama sehemu ya malipo. Kwa ambao watakosa basi fedha zao zitarudishwa hapo hapo.

Kwa watakaoshiriki kuharibu mnada, hawatorudishiwa fedha hizo na watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa mshindi atakayepata nyumba atatakiwa kulipa hapohapo 25% ya gharama yote ya nyumba na 75% ya gharama inayobaki atapaswa kulipa ndani ya muda wa siku 14.

Yono Auction Mart wametoa onyo kubwa kwa watakaohusika kwa namna yoyote kuharibu minada hiyo kuwa watakamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani kwa kuwa na nia ovu ya kukwamiha ukusanyaji wa kodi ya serikali
Share:

Waziri Mkuu Kassim majaaliwa Kufanya Ziara Ya Kikazi Mkoani Ruvuma .

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb) anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Ruvuma kuanzia tarehe 23 - 25 Novemba, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 22 Novemba 2017 na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Mheshimiwa Waziri Mkuu atawasili mjini Songea siku ya Alhamisi tarehe 23 Novemba, 2017 na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali katika Uwanja wa ndege Songea majira ya 7.00 mchana.

Baada ya kuwasili atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa na ile ya Chama Tawala Uwanja wa Ndege Songea. Kisha ataelekea Wilaya ya Namtumbo ambapo atafungua ghala la MIVARF, kuongea na Madiwani na watumishi wa Umma na baadaye ataongea na wananchi wa Namtumbo kwenye mkutano wa hadhara. 
Ijumaa tarehe 24 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu ataendelea na ziara yake kwa kuongea na wananchi wa kijiji cha Mchomoro kisha ataelekea Wilaya ya Tunduru ambapo atasalimia na wananchi wa vijiji vya Rahaleo,Milonde na Matemanga akiwa njiani kuelekea mjini Tunduru.

Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu atatembelea kituo cha Afya cha Nakayaya, ghala la kuhifadhia Korosho na kupata taarifa ya Chama Kikuu Cha Ushirika TAMCU. Jioni Mheshimiwa Waziri Mkuu ataongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini Tunduru katika uwanja wa michezo. Jumamosi tarehe 25 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu atahitimisha ziara yake mkoani Ruvuma na kurejea Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa Mndeme ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika mapokezi kuanzia uwanja wa Ndege Songea atakapowasili Aidha amewaomba wananchi kujitokeza kwenye maeneo yote ambayo Waziri Mkuu atapita na kwenye mikutano ya hadhara ili wapate fursa nzuri ya kumsikiliza Mheshimiwa Waziri Mkuu na kupokea maelekezo atakayoyatoa.
Share:

TANZANIA YAIPIGIA MAGODI MAREKANI,YAAMUA KUZIFATILIA MALI ZAKE,IKIWA NI PAMOJA NA BOMBARDIA MOJA ILIYO SHIKILIWA.

Image result for bombardier
Tanzania imeiomba Mahakama ya Jimbo la Columbia kutupilia mbali ombi la Stirling Civil Engineering la kutaka kusajili hukumu mbili za Mahakama ya Kimataifa Usuluhishi ili kampuni hiyo ya Uingereza ikamate mali nyingine za Serikali zilizopo nchini Marekani.

Stirling, ambayo ni kampuni ya ujenzi iliyokatishwa zabuni ya kujenga Barabara ya Bagamoyo kutoka eneo la Wazo Hill kutokana na kutekeleza mradi huo chini ya kiwango, ilishinda ksi iliyofungua kupinga kitendo hicho msuluhishi akaagiza ilipwe dola 38 milioni za Kimarekani.

Kampuni hiyo ilisajili uamuzi huo wa msuluhishi nchini Uingereza na Uholanzi na kufanikiwa kushikilia ndege aina ya Bombardier Q400 iliyonunuliwa na Serikali na sasa inataka mahakama isajili hukumu mbili za mwaka 2015 na 2016 zisajiliwe Marekani ili ipate nguvu ya kushikilia mali nyingine.

Lakini Serikali ya Tanzania imeamua kupambana na kampuni hiyo mahakamani kuizuia isiendelee kukamata mali zake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Law360, ambayo ni maalum kwa ajili ya habari za kisheria, Tanzania imewasilisha pingamizi, ikitaka mahakama hiyo isisajili hukumu hiyo ya Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi.

Katika hoja yake, Tanzania imesema mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria ya kushughulikia ombi hilo la Stirling.

Serikali inasema ina kinga dhidi ya hukumu mbili zilizotolewa na mahakamani nchini Uingereza na Uholanzi ambazo kampuni hiyo inaomba zitambuliwe pia Marekani, ikisema kuwa ondoleo hilo la kinga linalotolewa na Sheria ya Kinga ya Mataifa ya Kigeni, haiwezi kutumika.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Sheria ya Kinga ya Mataifa ya Kigeni inasema taifa la kigeni halitakuwa na kinga dhidi ya mamlaka ya mahakama ya Marekani katika mashauri yanayowasilishwa kwa ajili ya kuthibitisha tuzo za mahakama ya usuluhishi zinazoongozwa na makubaliano yaliyoidhinishwa na nchi yanayotambuliwa nchini Marekani.

Serikaloi inasema Stirling inataka kutambuliwa kwa hukumu za mahakama ya nje ili ziwe na nguvu, badala ya kuomba kutekelezwa kwa hukumu hizo.

“Kuna tofauti inayotambulika vizuri kati ya kuthibitisha tuzo ya msuluhishi, kwa upande mmoja, na kutambua hukumu ya mahakama ya nje, kwa upande mwingine,” tovuti hiyo inakariri hoja hizo za Serikali.

“ingawa tuzo ya msuluhishi na hukumu ya mahakama zinalingana kwa kiasi kikubwa, hata hivyo zina tofautiana.”

Kwa hiyo, Serikali inasema Stirling haiwezi kutumia mwanya huo, kuomba utekelezaji wa hukumu hizo.

Kampuni hiyo inadai kuwa kitendo cha Serikali ya Tanzania kukubali kwenda kwenye Mahakama ya Usuluhishi, kiliondoa kinga hiyo na kuipa yenyewe haki ya kulipwa fidia hiyo.

Mwaka 1999 Serikali iliipa kandarasi kampuni ya Impresa Ing. Fortunato Federici SpA (IFF) ambayo baadaye ilinunuliwa na Stirling, kukarabati barabara ya Wazo Hill-Bagamoyo, lakini baadaye ikatimuliwa.

Mwaka 2004 kampuni hiyo ilifungua kesi Mahakama ya Usuluhishi wa Kimataifa na hukumu ilitolewa mwaka 2009 na 2010, lakini Serikali haikulipa fidia iliyopendekezwa na kuilazimu kukazia hukumu Uingereza na Uholanzi.

Novemba 2015, mahakama nchini Uingereza iliridhia utekelezaji wa hukumu hiyo na Uholanzi ilifanya hivyo Desemba 2016
Share:

LIKE FB PAGE

bonyeza hapa

Total Pageviews

Blog Archive

Pages